Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo Instagram – Mwezi wa nne mwaka huu nilipata mualiko wa kushiriki tukio la Mwanamke CHUMA lililoandaliwa na @goldfmtanzania Kahama, Shinyanga.

Dada yangu Mhe @mboni_mhita alinipokea vizuri kweli kweli, tulikuwa naye mwanzo-mwisho na nakumbuka kumwambia Dada Mboni unastahili kuwa RC kama hauendi kugombea ubunge. Na kweli imekuwa hivyo kwa Rehema zake Mwenyezi Mungu.

Nichukue fursa hii kukupongeza wewe binafsi na vijana wote walioaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Niwasihi vijana wenzangu mliopata nafasi, pambaneni hizi nafasi mkazitumikie na sio nafasi kuwatumikia ninyi mkabweteka, mkawa wabinafsi. Vijana wanawahitaji mkashirkiane nao kuleta Maendeleo ya nchi yetu.

đź’šđź’šđź’šđź’šđź’šđź’š | Posted on 25/Jun/2025 13:17:21

Jokate Mwegelo

Check out the latest gallery of Jokate Mwegelo