Mimi na @salim_kikeke tumepata nafasi ya kukutana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Nishati ya @pertaminainternasionalep -Upande wa Utafiti- Ndugu Dadan Ramadan jijini Jakarta Indonesia. @pertaminainternasionalep kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania @tpdctz wanafanya kazi pamoja katika mradi wa gesi wa Mnazi Bay. Ushirikiano baina ya Petramina na TPDC ambayo yote ni mashirika ya umma, unahusisha pia kuwajengea uwezo zaidi wataalam wa TPDC katika sekta ya nishati kwa kupata mafunzo nchini Indonesia. Indonesia ni miongoni mwa mataifa yaliyo na uzoefu mkubwa katika masuala ya nishati hasa gesi ya LNG. Gesi hiyo ni miongoni mwa nishati safi ambazo dunia inazipigia chapuo katika kupambana na hewa chafu. Tanzania inalenga kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Rais wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa kushinikiza matumizi ya nishati safi. Thank you to @indonesiaindaressalaam for making this mwet up possible.