Wema Sepetu Instagram – Leo tukiwa Simiyu tumepata fursa ya kutembelea moja kati ya Mradi mkubwa sana wa Maji hapa Bariadi… Itoshe kusema Kazi imefanyika hapa na napenda kumpa pongezi za dhati kaka yangu @jumaa_aweso Waziri wa Maji… Kiukweli sidhani kama kuna haja ya kuja kuwa na Waziri mwingine kwenye idara ya Maji… Chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan… Historia inaenda kuandikwa Simiyu… Mradi huu mkubwa sana ambao umegharimu zaidi ya Billion 440 unaenda kutatua matatizo ya maji kwa asilimia kubwa kwa Wananchi…. Wema wa Mama unaendelea kuonekana kwa vitendo kabisa… Pichani nilipata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Mbunge Simon Songe Lusengekile nae alikuwa na Mengi ya kuelezea kuhusu Maendeleo yanayoendelea kufanyika katika Idara ya Maji, Elimu na Afya… Kazi na Iendelee.. | Posted on 15/Jun/2025 23:53:57
Check out the latest gallery of Wema Sepetu



