Frida Amani

Frida Amani Instagram – Ninayo furaha kubwa kupata heshima hii, na ninakubali rasmi uteuzi huu kama Balozi wa kwanza wa UNEP @unep katika kusimamia Urejeshwaji wa Mifumo ya Ikolojia. Heshima hii ni kubwa kuliko ninavyoweza kueleza. Mazingira yamekuwa msingi wa ustawi wetu na kuyaona yakidhoofika kumezidi kuniaminisha kuwa kila mmoja wetu, mimi nikiwemo, tuna jukumu la kurejesha tunachopoteza.

Ninaishukuru UNEP kwa kuniamini na kunipa nafasi hii muhimu, na kwa kutambua nguvu ya sanaa, utamaduni na vijana katika kuleta mabadiliko ya kimazingira.

Kupitia nafasi hii, najitoa kutumia sauti yangu, jukwaa langu na ubunifu wangu kuelimisha jamii, kuhamasisha utunzaji wa mazingira, na kuhamasisha hatua ndani ya Afrika na zaidi. Nitaendelea kuwaunga mkono wanawake, kuinua vijana na kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika kila kazi ninayofanya kuanzia muziki hadi miradi ya jamii.

Huu si tu utambulisho; ni mwito wa kutumikia. Pamoja, tutarejesha mifumo ya ikolojia, kulinda mustakabali wetu, na kujenga kizazi kinachoelewa kuwa kuirudisha asili katika uhai si hiari ni wajibu.

Asante sana kwa heshima hii kubwa.

Good morning , Generation Restoration.

I am deeply honored to accept this appointment as the first-ever UNEP Goodwill Ambassador advocating for Ecosystem Restoration.

I am grateful to UNEP for trusting me with this responsibility and for believing in the power of art, culture, and youth to drive meaningful environmental change.
We are Generation Restoration
I AM GENERATION RESTORATION. | Posted on 02/Dec/2025 14:13:49

Frida Amani
Frida Amani

Check out the latest gallery of Frida Amani