Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo Instagram – Kicheko Cha Mama Na Vijana wake wa Kazi 🙂‍↔️

Kama anavyosema ndugu yangu mchekeshaji mahiri @saidsaid._ wakati wa Mungu ni wakati sahihi!!!

Ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani Tanga ikiwa tumeingia siku ya pili imekua na mafanikio makubwa na motisha kwetu Vijana wa CCM. Hapa ni baada ya Kuzima Zote Na Kuwasha Kijana Wilaya ya Korogwe- home kabisa!!!

Tunatambua kazi kubwa unayofanya kwa Taifa letu na ndio maana wakati wote Vijana tumekua mstari wa mbele kuitetea Imani ya CCM na Serikali yako.

Tunakushukuru sana Mhe. Rais kwa kuendelea kutuamini sisi Vijana, nasi tunakuahidi kuwa tutaendelea kukuunga mkono na kusimama bega kwa bega na wewe kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu huu wa 2025 tunashinda kwa kishindo. | Posted on 24/Feb/2025 23:07:17

Jokate Mwegelo
Jokate Mwegelo

Check out the latest gallery of Jokate Mwegelo