Jokate Mwegelo Instagram – Kwenye miradi inayotekelezwa na serikali; vijana ni wawezeshaji na wanufaika wakubwa. Wawezeshaji kwa maana ya nguvu kazi na taaluma inayotumika inatoka kwa vijana na wanufaika maana baada ya kukamilika kwa miradi hii sisi vijana tunaitumia kujiendeleza kiuchumi na kijamii.
Daraja hili la JP Magufuli halihusiani tu na usafiri na usafirishaji bali daraja hili ni fursa.
Rai yangu ili kuendelea kutambua umuhimu wa kundi hili la vijana kwenye kutekeleza miradi ya miundombinu nchini ni wakati muafaka wa kuwa na Mpango wa Kitaifa wa Kuwezesha Vijana Kushiriki Ujenzi wa Miundombinu. Ikagusia maeneo ya kuwa na kanzi data ya wataalamu vijana sambamba na uwezeshaji wao kushiriki kwenye miradi hii mikubwa. | Posted on 25/Jun/2025 00:08:22



