Hamisa Mobetto Instagram – 🏆🏅Tunajivunia kutangazwa kuwa Banda la Tatu Bora kwa Ujumla katika Maonesho ya Sabasaba 2025!
Huu ni ushahidi kuwa safari yetu ya kuwa mshirika wa kweli kwa wateja katika zama hii ya kidigitali inaendelea kwa mafanikio makubwa.
Tuzo hii imekabidhiwa na Mgeni Rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dr. Hussein Ali Mwinyi, na kupokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Pierre Canton Bacara.
Tunaamini mafanikio ya mteja ndiyo mafanikio yetu na hii ni hatua nyingine kuelekea huko.
Asante kwa kuendelea kutembelea banda letu la Yas kwa kuamini kuwa kwenye kuanza safari yako ya mafanikio pamoja nasi.
#YasSabasaba2025 #AnziaUlipoNaYas | Posted on 08/Jul/2025 14:01:02


