Hamisa Mobetto Instagram – Ilikuwa siku ya kipekee na Mheshimiwa Balozi wa Ufaransa @as.ave katika Ubalozi wa Ufaransa hapa Tanzania @franceintanzania tulijadiliana kuhusu kukuza sekta ya ubunifu, mitindo, na sanaa 🇹🇿🇫🇷✨
Tukabadilishana mawazo juu ya ukuaji wa vipaji vya ndani, huku tukigusa maeneo yenye umuhimu mkubwa kwa vijana kama elimu, biashara na teknolojia.
Tuliwasilisha utambulisho wetu wa mitindo kama njia ya kueleza ubunifu wetu, lakini pia kuonyesha namna sanaa inaweza kuwa daraja la maendeleo.
Tunashukuru kwa mapokezi mazuri na maono ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano na kuinua kizazi kijacho. 🤝🎨👗📚
L’union fait la force. 🤍
@as.ave @franceintanzania @iammangoma | Posted on 12/Jul/2025 18:58:24



