Jokate Mwegelo Instagram – Nitumie fursa hii kama Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Msalato Secondary School iliyopo Dodoma kuwapongeza wahitimu wote wa Kidato cha Sita, Uongozi wa Shule na Walimu kwa matokeo mazuri yanayoendeleza sifa za kihistoria na jina jema la Shule yetu ya Msalato. Kongole pia kwa wazazi na walezi kwa mafanikio haya.
Aidha, kwa upekee wake niwapongeze pia walimu, wanafunzi na uongozi mzima wa shule iliyopewa jina langu na viongozi wangu wa Kisarawe- Pwani, Jokate Mwegelo Secondary School kwa kuendeleza falsafa njema ya Tokomeza Zero Kisarawe kwa vitendo!!!
Nawatakia mabinti wote kila la kheri na hatua zinazofuata katika kujiendeleza ❤️❤️❤️❤️❤️❤️ | Posted on 10/Jul/2025 10:20:47



