Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo Instagram – Jana nilipata wasaa wa kutembelea Chuo chetu cha UVCCM Tunguu aka DAMBWE kilichopo Zanzibar na kukagua maendeleo ya madarasa, mabweni na miradi ya kimkakati.

Nilifanya ukaguzi huo nikionyeshwa maendeleo hayo na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi ambapo alinionesha miradi ya shamba la mahindi, nyanya, pilipili hoho na miti ya matunda ikiwemo papai ambayo hii yote imeanza kuleta faida kwa kuuza kwa wananchi.

Pia nimejionea maendeleo ya mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai ambayo yanauzwa kwa Wananchi na tayari UVCCM Afisi Kuu Zanzibar imekaribisha wananchi kununua biashara hizo.

Nimewapongeza viongozi wote kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa chuo hicho na zaidi Mwenyekiti wetu Cde. Mohamed Ali Kawaida kwa kuhamasisha viongozi wa Serikali na Chama na wadau mbalimbali wa chuo chetu kushirikiana nasi katika kufanya maboresho haya tunayoyaona.

@comrade_kawaida @abdimahmoud @uvccm_tz @uvccm_zanzibar | Posted on 09/Jul/2025 15:50:15

Jokate Mwegelo
Jokate Mwegelo

Check out the latest gallery of Jokate Mwegelo