Jacqueline Wolper Instagram – Kuna ule usemi unasema NABII hakubaliki kwao…Kuna Mtumishi mmoja wa Mungu kuna video yake imetembea sana huku mitandaoni, halafu baadhi ya watu wamechukulia ni kama content kwenye kurasa zao! Kitu ambacho naona sijapenda kwa mtazamo wangu sifurahishwi na aina hiyo ya masihara hivi jamani kwa Mungu kuna linaloshindikana kweli au IMANI zetu zipo wapi, Mungu anaweza akafanya njia hata pasipo na njia, anaweza akafanya chochote kwenye hali ambayo wewe unaweza kuona haiwezekani..hawa wabeba maono tujifunze namna ya kuwaheshimu kwasababu kuna vitu Mungu ameweka ndani yao ambavyo hatuwezi kuelewa kwa macho ya nyama..Miujiza ipo na watu wanakutana na miujiza kila siku msione masihara lakini watu wanatendewa katika hali ambazo si za kawaida.Na siku zote watu wenye maono huwaga wanachukuliwa poa unaweza kuwaona kama watu wa kawaida au kuwadharau lakini hiyo nguvu aliyoweka Mungu ndani ya mbeba maono ina uwezo hata wa kukomboa TAIFA, ina uwezo wa kubadilisha historia na maisha ya watu..wengine tuna ushuhuda nyingi za kushangaza lakini muda na kibali bado hatujapata cha kushuhudia…tuache kubeza imanı za watu na pengine kuna watu kibao wanamuona Mungu kupitia hao mnaowaletea masihara..nimejifunza hilo swala la kuamini pale niliposoma WAEBRANIA 11:1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 🙏🏿 | Posted on 08/Aug/2025 15:10:06
Check out the latest gallery of Jacqueline Wolper



