Elizabeth Michael

Elizabeth Michael Instagram – Dear Tanzania 🇹🇿

Samahani kwa kukuchukulia poa,samahani kwa kutothamini yale mazuri yote uliyotupa bila malipo yoyote…TUMEKUKOSEA NA TUMEKUFELISHA 😭 hatuna budi kukubali hivyo..!

Katika yote,binafsi bado nina imani na wewe,najaribu kujishawishi kwamba pengine ulitaka kutupa funzo la kujua thamani ya yale yote tuliyoyaona ya kawaida sana….TUMEJIFUNZA (Japo kwa njia ngumu sana) ila TUMEJIFUNZA
Kwa Mapenzi ya MUNGU,tupe nafasi nyingine…tuko tayari😭tumekukosea na tumejifunza kweli kila mmoja wetu kwa upande wake…bila kujali tofauti zetu za umri,elimu,itikadi n.k.

Kwa Mapenzi ya MUNGU,tuwezeshe kuponya mioyo yetu kila mmoja sawasawa na majeraha yake,turudishie tena ule UPENDO,AMANI na MSHIKAMANO,turudishie ile ya familia moja ya kuweza kuwa na mitazamo tofauti lakini bado tukawa familia moja,ile familia yenye kuweza kukubaliana kutokukubaliana kwa hekima….na kama kwa mara nyingine tena kama itakubidi kutupa mafunzo (maana hatutaacha kujifunza) basi tuchagulie namna rafiki zaidi🙏

Wewe Ndo Asili,Nchi yetu,Ardhi yetu,kimbilio letu…umebeba historia zetu…umebeba baraka zetu na sio laana..!
Nimetamani sana kukaa kimya,kujisahaulisha lakini nimegundua njia moja wapo ya kupona ni kukubali TUMEKUKOSEA na kurekebisha kuanzia sasa.

Dear TANZANIA,tuombee rehema za MUNGU,huruma ya MUNGU lakini zaidi HEKIMA yake yenye kuzidi uwezo wetu wa kibinadamu 🇹🇿 ❤️ | Posted on 04/Nov/2025 20:50:25

Elizabeth Michael
Elizabeth Michael

Check out the latest gallery of Elizabeth Michael