Rose Ndauka

Rose Ndauka Instagram – Huu Mwaka nataka kufanya sana kazi,Kama kipindi cha miaka saba nyuma,hapo nilikuwa nafanya kazi hadi najionea huruma…Kidogo familia na malezi yalinifanya nipunguze speed..
Na wewe kama malengo yako ya Mwaka huu ni kufanya kazi sana,Ni muhimu na vyema kuna vitu kuvizingatia

1.Mtangulize Mwenyezi Mungu kwenye mipango yako.

2.Hakikisha Mipango yako na juhudi zako zinaendana.

3.Usilete mapenzi binafsi kwenye kazi(Hii itakuharibia kazi)

4.Ogopa anaejifanya kukupenda ili afanye kazi na wewe(inaweza kukucost)

5.Jitahidi kila baada ya muda flani kuhakiki unachokifanya

6.Kumbuka kwenye kutafuta kuna muda kuna kupoteza,ikiwa hivyo usipanick mshukuru Mungu maana yeye ana makusudi ya kila japo

7.kuhakikisha unafanya kazi kwa weledi ili wengi wavutiwe na kazi yako.

8.Hakikisha unalinda Thamani yako na unachokifanya..

9.Fanya kazi,pambana usikate tamaa hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi.USIKATE TAMAA

10.Mtangulize Mungu kila muda kila wakata(Maana sisi tunapanga na yeye anapanga) | Posted on 11/Jan/2026 15:15:50

Rose Ndauka
Rose Ndauka

Check out the latest gallery of Rose Ndauka