Hamisa Mobetto Instagram – Siku ya jana nimeheshimika kuwa sehemu ya uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF 2025), tukio lililozinduliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi. @dr.hmwinyi
Hotuba yake imegusa moyo wangu. Akisisitiza dhamira ya Serikali kushirikiana na sekta binafsi, wajasiriamali na wawekezaji ili kuhakikisha mazingira bora ya biashara na uwekezaji hapa nyumbani.
Kwa mwanamke ambaye ana ndoto kubwa, haya ni mazingira ambayo yanatia moyo. Maendeleo ya Taifa huanza pale ambapo kila mmoja anapata nafasi ya kushiriki.
Nimejifunza, nimehamasika, na zaidi ya yote, najivunia kuwa Mtanzania.
Kwa pamoja tunaipeleka Tanzania mbele kwa ubunifu, kwa mshikamano, na kwa uzalendo. 🇹🇿
#DITF2025 #MadeInTanzania #HamisaMobetto #Sabasaba49 #Ujasiriamali #VijanaNaBiashara | Posted on 08/Jul/2025 20:18:21



